32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

FANYA HAYA KUMDHIBITI MTOTO MWENYE HASIRA

NA AZIZA MASOUD,

TAFITI mbalimbali za wanasaikolojia zinaonyesha kuwa, hasira za mtoto, hasa wenye umri kati ya mwaka mmoja na kuendelea, zinatokana na mtoto husika kuhifadhi baadhi ya mambo kichwani, hasa mabaya.

Kwa sababu anakuwa hana uwezo wa kuyatatua kwa umri alionao, anakuwa mtu wa kuishi na kinyongo kwa kuweka vitu moyoni.

Mtoto inapotokea akipata makwazo kidogo kutoka kwa mzazi ama mlezi wake na watu wanaomzunguka huonyesha kuwa mtu mwenye hasira ya kiwango cha juu, hata kama kosa alilotendewa ni la kawaida.

Mzazi je, uliwahi kujiuliza kwa nini mtoto wako mdogo anakuwa na hasira. Je, umewahi kujiuliza mtoto wako anatoa wapi hasira hizo, jibu hapa.

Umewahi kufikiria njia za kumsaidia ili mtoto wako arudi katika hali ya kawaida anapokuwa katika hali hiyo.

Mtoto wako mwenye umri wa miaka miwili   anapokasirika na kuanza kupiga kelele, anapigapiga miguu chini kwa kishindo, na kujigaragaza chini, mara nyingi wazazi huwa wanajiuliza “Mtoto wangu yuko sawa kweli?

Katika kipindi hicho mzazi anakuwa anategemea zaidi kufanyiwa baadhi ya vitu kutoka kwa mtoto kuliko kumfanyia yeye.

Kunapokuwa na mabadiliko hayo ni ngumu kwa mtoto kuyakubali kirahisi, usidhani kwamba mtoto atakuwa na mabadiliko hayo kwa urahisi.

Mlipuko wa hasira unapoanza mshikilie mtoto wako (ikiwa inawezekana) na, bila kumuumiza, mzuie asijigaragaze. Usimfokee mtoto wako.

Subiri mpaka hali itulie na baadaye mtoto atatambua kuwa kulipuka kwa hasira hakukumsaidia kwa njia yoyote.

Tenga mahali utakapomuweka mtoto wako wakati akiwa na hasira. Mwambie kwamba atatoka humo mara tu anapotulia, na kisha umwache humo.

Ikiwa mtoto wako huwa anapandwa na hasira mbele za watu, mwondoe eneo alipo na wala usimpe anachotaka kwa sababu tu amekasirika mbele za watu.

Ukimpa kitu kwa wakati huo inaweza  kumfanya afikiri kwamba ikiwa atakuwa na hasira, anaweza kupata chochote anachotaka.

Unapomkuta kwenye hali ya hasira ni vema ukamuuliza sababu za yeye kufanya hivyo, kama ni tatizo jaribu kumwelewesha njia sahihi uliyopanga kuitumia kwa ajili ya kumsaidia.

Mzazi ni vema ukamsoma mtoto anapokuwa katika hali ya hasira na kujua jinsi ya kumtuliza ili asilete shida anapokuwa mbele ya macho ya watu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles