25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Fally atua nchini, kutikisa Dar na Mwanza

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Mkali wa muziki wa Dansi kutoka Congo, Fally Ipupa, amewasili nchini Tanzania akiwa na kundi la wanamuziki 35 kwa ajili ya kufanya maonesho katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam Oktoba 9, na baadae ukumbi wa Malaika katika Jiji la Mwanza Oktoba 13.

Akizungumza baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam, Fally amesema anao uzoefu wa kutosha na wa muda mrefu katika muziki wa Dansi, hivyo Watanzania watarajie burudani ya nguvu kutoka kwake sambamba na nyimbo zake mpya.

“Nimekuja na vitu vingi vipya, kutakuwa na Suprise, hivyo Watanzania watafurahi sana, niwahakikishi mashabiki wa muziki wa dansi watakaokuja Mlimani City na baadae katika Jiji la Mwanza watafurahi, mimi na wanamuziki wangu tumejipanga, umejiandaa kutoa burudani, niwaombe tu kateni tiketi mapema,”amesema.

Ameongeza kuwa anatambua hajaja Tanzania kwa zaidi ya miaka 10, hivyo kuna nyimbo nyingi ambazo amezitoa lakini anawaachi mashabiki ndio wataamua wanataka kusikia nyimbo gani kutoka kwake ingawa amejiandaa vya kutosha.

“Niwahakikishie nitafanya Shoo ambayo sijawahi kufanya hapa Tanzania, njooni Mliman City siku ya Jumamosi, kutakuwa na Sebene na Rhumba kali.”

Kuhusu idadi ya msafara ambao amekuja nao, Fally Ipupa amesema kutoka Paris Ufaransa amekuja na jumla ya watu nane na wengine 24 wataingia usiku wa leo kwa Ndege la Ethiopia wakitoa Kinshansa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Prime Time Promotion, God Kusaga amesema Fally tayari amewasili nchini na onesho lake la kwanza litafanyika Jumamosi ya Oktoba 9, katika ukumbi wa Mliman City na baada ya hapo atakwenda Mwanza katika ukumbi wa Malaila Oktoba 13, mwaka huu ambayo itakuwa siku ya mkesha wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Julius Nyerere .

“Maandalizi yamekamilika, tunawaomba mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi, mashabiki wa Fally Ipupa kukata tiketi mapema kwani zimebakia chache kumalizika, tunaamini atafanya Show nzuri na kuutangaza utalii wetu,” amesema Kusaga.

Msisimko ni mkubwa sana na milango itakuwa wazi kuanzia saa 12 jioni, amesisitiza Kusaga.

Ameongeza kuwa ujio wa Fally Ipupa watanzania wategemee shoo kubwa ya kisasa kwa Dar es Salaam na Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles