25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Faida za tamasha la muziki la Sauti za Busara nchini zawekwa wazi


Bethsheba Wambura na Elizabeth Joachim, Dar es Salaam

Uongozi wa tamasha la 16 la Kimataifa la Muziki la Sauti za Busara linalotarajiwa kufanyika Februari 7 hadi 10 katika Ukumbi wa Ngome Kongwe, visiwani Zanzibar, umeweka wazi idadi ya wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha hilo na faida inazopatikana kwa nchi na wasanii kwa ujumla.

Tamasha hilo linalofanyika kila mwaka kwa mwaka huu litakuwa na kauli mbiu isemayo ‘Potezea Rushwa Sio Dili’.
Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud amesema Zanzibar itapokea wapenzi wa muziki kutoka kila kona ya dunia watakaoungana kusheherekea sauti za muziki mtamu kutoka Algeria hadi Zimbabwe na Cape Town Hadi Casablanca.

Mahmoud amewataja wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo kutoka Tanzania ni pamoja na Fid Q, Damian Soul, Kikundi cha Mkubwa na Wanawe, Stone Town Rockers, Tausi Women’s Taarab, Rajab Suleiman & Kithara na Afrigo Band.

Wasanii wengine nchi wanazotoka kwenye mabano ni Akello na Eli Maliki (Uganda), Fadhilee Itulya na Shamsi Music (Kenya), BCUC (Afrika Kusini), Mokoomba (Zimbabwe), Faith Musa (Malawi), HobaHoba Spirit (Morocco), M’ToroChamou (Mayotte), Tune Recreation Committee (Afrika Kusini) Ithrene na Ifrikya Spirit(Algeria), Asia Madani (Sudan na Misri), Sofaz na Dago Roots na wengine wengi.

“Pamoja na hao ila tamasha la mwaka huu tunaangalia sana vipaji vichanga ambapo kutakuwa na kikundi cha Wamwiduka Band kutoka Mbeya na S Kide anayeimba Singeli ambao ndio muziki halisi wa Tanzania na hivi karibuni utafika duniani kote,” amesema.

Tamasha hilo limedhaminiwa na ubalozi wa Norway, ubalozi wa Uswisi kwa Tanzania na Zambia, Umoja wa Ulaya, Africalia, Balozi za Ufaransa na Ujerumani, Pro Helvetia, TV-E na Efm Radio, Zanlink, Mozeti, Shirika la ndege la Ethiopia, African Movie Channel, Shirika la Habari Zanzibar (ZBC) na wengine wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles