Ma-RPC waliotumbuliwa na Lugola wachunguzwa, nafasi zao zikichukuliwa

0
1138

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Makamanda wa Polisi wa mikoa mitatu waliotumbuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, wiki iliyopita,  wamehamishiwa Makao Makuu ya Polisi kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa dhidi yao.

Makamanda hao na mikoa yao kwenye mabano ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ramadhan Ng’anzi (Arusha), Kamishna Msaidizi, Emmanuel Lukula (Temeke) na Kamishna Msaidizi, Salum Rashid (Ilala).

Hatua hiyo imechukuliwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, ambaye amefanya mabadiliko ya makamanda hao ambapo makamanda wa polisi wa mikoa hiyo watateuliwa hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here