Makampuni nguli Exim Bank ya nchini Tanzania na shirika la ndege la Oman yaungana kutoka punguzo la aina yake kwa wateja wa benki hiyo. Kwa mwaka mzima, wateja wa huduma ya Preferred Banking ya Exim watapata punguzo la asilimia 15% kwa safari zote za kutoka nchini zinazofanywa na shirika la Oman Air.
Akizungumza ofisini kwake, Meneja masoko wa Exim Bank Bi Mariam Mwapinga alisema ‘Punguzo hilo litadumu kwa miezi 12 kwa wateja watakaokata tiketi za ndege kati ya mwezi Septemba 2016 na Septemba 2017, na kusafiri kabla ya mwezi Desemba 2017.
Kuhusu kiwango hasa cha punguzo hilo, Bi Mwapinga alisema ‘Punguzo ni asilimia kumi na tano, kwa mfano kama gharama ya tiketi ni shilingi milioni moja, basi utapunguzi wa laki moja na nusu’.
Alipoulizwa juu ya wateja wapya, kama nao wanaweza kupata punguzo hili, Bi Mwapinga alisema ‘Ndio wanaweza, wanachotakiwa ni kufuata hatua chache tu kuweza kujiunga na familia yetu. Kwanza watatakiwa kutembelea tawi lolote la Exim Bank na kufungua akaunti chini ya huduma ya Preferred Banking.’
Aliendelea kutoa maelezo, ‘Huduma ya Preferred Banking ni huduma ya kipekee, yaani unaweza kupata huduma zote za kibenki kwa kujinafasi. Ukiwa na akaunti hii utapata meneja uhusiano, maalumu kwa ajili ya kopekee, viwango vyenye upendeleo wakati ukibadili fedha za kigeni, punguzo maalumu kwa makampuni washirika kama vile kama Ramada Hotels na maduka ya Shoppers. Pia utapata punguzo la asilimia 15 unaposafiri na ndege za Oman Air kuelekea safari zaidi ya 50 duniani.’
Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kujiunga na Exim Preferred Banking na kupata punguzo hii, fika katika tawi lililo karibu nawe au piga simu namba +255 784 107 600. Pia unaweza kutuma barua pepe kwenda [email protected] au tembelea kurasa zao za Facebook na Twitter @eximbanktzna @Exim_BankTz.