BRUSSELS, Ubelgiji
RAIS wa Kamisheni ya Nishati wa Jumuiya ya nchi za Ulaya,EU, Maros Sefcovic, amesema kwamba tayari ameshafanya mazungumzo ya awali na nchi za Urusi na Ukraine ya kuongeza mkataba wa gesi kuendelea kupitia Ukraine pindi mkataba wa sasa utakapomalizika ifikapo mwakani.
Sefcovic alitoa kauli hiyo juzi katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza, Reuters na akasema kuwa mazungumzo ya kina yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
“Tumeshafikia makubaliano ya wali na washirika wetu hao wawili, Ukraine na Urusi na tumewaarika kufanya mazungumzo ya kina,”alisema Rais huyo wa Kamisheni ya Nishati Ulaya.
“Mazungumzo ya kina yatafanyika hivi karibuni na jambo na muhimu litakuwa ni kuhusu kuendelea kuagiza gesi na tunataka iendelee kupitia Ukraine mara baada ya mkataba huu kumalizika mwakani,”aliongeza, Sefcovic
Alisema kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin naye alishamuhakikishia kuwa Serikali ya Moscow, tayari imeshafanya mazungumzo na Ukraine ili gesi hiyo iendelee kupitia nchini humo, baada ya wiki iliyopita kukutana na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.