24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

EU kuendeleza utekelezaji makubaliano ya nyuklia Iran

BRUSSELS, UBELGIJI

MWANADIPLOMASIA Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Federica Mogherini, ameeleza dhamira ya wazi ya umoja huo  na wanachama wake 28 kuendelea na utekelezaji kamili wa makubaliano ya nyuklia na Iran.

Mogherini ambaye ni mwakilishi wa masuala ya kigeni wa EU, alitoa kauli hiyo juzi wakati alipokutana na mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa umoja huo  kwa  mazungumzo ya kawaida na  kujadili juu ya hali ya Libya na mkataba wa nyuklia  wa Iran.

Baada ya mkutano  huo, mwanadiplomasia huyo alikutana na mawaziri wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani pamoja na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Mike Pompeo na kutoa msimamo huo wa kuunga mkono mkataba na kuionya Marekani dhidi ya kuongeza mzozo uliopo.

Mazungumzo hayo yanafuatia onyo lililotolewa wiki iliyopita na Rais wa Iran, Hassan Rouhani ambaye alieleza kwamba Tehran itaweza kurudia kurutubisha uranium ya kiwango cha juu kama EU, China na Urusi  hazitaunda mpango wa kuzuia adhabu ya vikwazo vya Marekani kwa mabenki yake na sekta za nishati.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano huo,  Mogherini alisema kwamba mawaziri walimweleza Pompeo wasiwasi wao mkuu ulikuwa ni kudumisha amani na utekelezaji wa mkataba wa nyuklia wa Iran wa mwaka 2015.

Onyo la EU kuhusu kuongezeka hali ya mvutano limetolewa wakati Marekani ambayo ilijitoa katika  mkataba wa kimataifa kupunguza nia ya Iran kumiliki silaha za nyuklia imepeleka manuwari ya kubeba ndege za kivita ya USS Abraham Lincoln na ndege nne za mashambulizi aina ya B-52  katika eneo la Mashariki ya Kati katika kujibu wasiwasi kwamba Iran huwenda inapanga shambulizi dhidi ya vituo vya Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles