24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kiir aahidi kufanya kazi na upinzani

JUBA, SUDAN KUSINI

RAIS Salva Kiir amesema kwamba atatumia rasilimali zote zilizo kwenye mhimili wake kuleta amani na uthabiti na ametoa wito kwa vyama vyote kufanya kazi pamoja ili kurejesha amani na kuruhusu watu kutembea huru katika maeneo ya nchi.

Pia amewasihi wabunge na maofisa wengine kuunga mkono utekelezaji wa mkataba wa kurejesha amani nchini hapa ambao ulitiwa saini mwaka 2018.

Katika hotuba yake ya juzi wakati wa kufunguliwa tena bunge la muda la kitaifa mjini hapa, Kiir alionya kwamba nchi haitasonga mbele hadi Serikali na upinzani waweke kipaumbele utekelezaji wa mkataba.

 Alitoa wito kwa vyama vyote kufanya kazi pamoja kurejesha amani na kuruhusu watu kutembea huru kwenye maeneo. 

“Nchi yetu ipo njia panda. Ninasimamia amani na uthabiti na ninakataa kabisa vita. Serikali yangu kwa kutambua hilo, inatumia rasilimali zote kwa mamlaka yake kwa sababu ya kuelezea amani na uthabiti katika mila zetu na jukumu la dini la kuleta amani kwa watu wetu,” alisema Kiir.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya Marekani (VOA), hotuba hiyo ya Rais Kiir aliwakuna wabunge, wanadiplomasia na maofisa wengine waliokuwepo wakati aliposema kwamba yupo tayari kufanya kazi na makundi ya upinzani kurejesha uthabiti na hivyo kupigiwa makofi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles