27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Esther Bulaya atoa msaada hospitalini

Esther Bulaya
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Mara, Esther Bulaya.

Na Shomari Binda, Bunda

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Esther Bulaya (CCM), ametoa msaada wa shuka 200 kwenye Kituo cha Afya cha Manyamanyama wilayani Bunda ikiwa ni jitihada za kuchangia kituo hicho kilicho kwenye mchakato wa kutangazwa kuwa hospitali ya wilaya.

Akikabidhi msaada huo, Esther alisema yeye kama mkazi wa Manyamanyama ameguswa na masuala ya kijamii na kuamua kuchangia vifaa hivyo.

Alisema alipotembelea kituo hicho siku za nyuma alipewa taarifa ya upungufu mkubwa wa mashuka kwenye kituo hicho na kusababisha wagonjwa kulala kitandani bila shuka ya kutandika na kujifunika.

Alisema taarifa hizo zilimsononesha na kuamua kujibana katika matumizi yake na kupata fedha za kununua shuka 200 zenye thamani ya Sh milioni nne ambazo anaamini zitapunguza adha hiyo.

Akipokea msaada huo, Mganga wa Wilaya ya Bunda, Charles Mkombe, alisema msaada huo umekuja wakati muafaka kwa sababu kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mashuka 640 ili kukidhi mahitaji.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Hongereni kwa kurudisha hela za walala hoi kwa mbinu nyingine za kusema mnatoa msaada basi msijitangaze mkifanya hivyo nia yenu nini hapo baadae….nyie wanasiasa wa Tanzania mnatutia aibu huku nje.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles