26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

UTPC yataka ukatili uwekwe wazi

Abubakar Karsan
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan

Na Benjamin Masese, Mwanza

WAANDISHI wa habari nchini wameshauriwa kutumia kalamu zao vizuri katika kipindi hiki ambacho taifa linakabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia na mauaji ya vikongwe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan, aliyasema hayo wakati akifungua semina kwa waandishi wa mikao ya Kanda ya Ziwa juu ya ukatili wa kijinsia.

Karsan alisema vitendo vya ukatili wa kijinsia na mauaji ya vikongwe vinaendelea ndani ya mikoa ya Kanda ya Ziwa huku jamii ikiona ni jambo la kawaida.

“Nichukue fursa hii kutoa onyo kali kwa waandishi popote pale walipo nchini ambao huandika habari za upotoshaji na uchonganishi, hii ni sehemu ya uchochezi na kuleta ugonjwa ndani ya jamii ambao dawa yake haipatikani kwa urahisi, tunaelekea kwenye uchaguzi naomba waandishi tusitumike kwa masilahi binafsi ya watu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valeria Msoka, alisikitishwa na taarifa zilizowasilishwa na waandishi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhusu wanawake wanavyofanyiwa ukatili wa kutobolewa macho kwa imani za kishirikina.

Kutokana na taarifa hizo, Msoka amewataka waandishi wa mikoa hiyo kuunda umoja wa kupambana na vitendo hivyo kwa kuandika habari na makala zinazobainisha chanzo cha unyama huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles