27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

ERB yatakiwa kuja na mwarobaini wa uhaba wa mafundi sanifu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Miundombinu, Balozi Mhandisi Aisha Salim Amour ameielekeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini(ERB) kupeleka serikalini mpango mkakati utakaotatua changamoto za uhaba wa mafundi sanifu ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa elimu na ajira.

Balozi Mhandisi Amour ametoa maagizo hayo Mei 4, 2023 wakati akifungua mkutano mkuu wa tano wa mwaka wa mafundi sanifu uliowakutanisha washiriki zaidi ya 500 kutoka mikoa mbalimbali nchini uliofanyika jijini Mwanza hadi Mei 5,2023.

“Naielekeza ERB kuhakikisha kwamba mfumo huo watakaouleta uwavutie mafundi sanifu na hivyo kuwafanya wabaki kwenye tasnia hiyo badala ya kuhamia tasnia nyingine kwani wengi tunaelewa kwamba mafundi sanifu wengi wameacha kufanya kazi walizosomea wamejikita kwenye fani zingine kutokana na matatizo mbalimbali yaliyotokea katika mfumo wa ajira,”alisema.

Aidha, ameisisitiza ERB kuendelea kusajili mafundi sanifu wenye sifa stahiki na kuwaunganisha katika miradi mbalimbali huku pia akiwataka mafundi hao kujiendeleza ili waweze kukithi vigezo vya soko hasa kwenye miradi mikubwa ya kitaifa ikiwemo bomba la mafuta kwa kuwa serikali inahitaji ajira nyingi zibaki nchini.

“ERB fanyeni juhudi maalumu kuhakikisha hatupotezi ajira kwa kuwapa mafundi sanifu wetu wa ndani, bodi iendelee kujenga uelewa kwa mafundi sanifu makazini pamoja na vyuoni juu ya umuhimu wa kusajiliwa na kuwakumbusha waajiri kufuata sheria kwa kuajiri mafundi sanifu waliosajiriwa na kuweka kigezo cha usajiri kwenye ajira,” amesisitiza Balozi Mhandisi Amour na kuongeza:

“Hili ni muhimu sana kwenu nyie mafundi sanifu, kwa sababu unaposajiliwa inamaana unatambulika hivyo usajili huo utawaongezea nguvu kwa waajiri na serikali inapopanga mipango ya kuwaendeleza itakuwa na takwimu sahihi,” amesema.

Nae, Msajili Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Benard Kavishe aliwataka wahandisi na mafundi sanifu kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao ambapo alieleza kwamba siku ya mafundi sanifu ilianzishwa mwaka 2019 na kwamba lengo la maadhimisho hayo ni pamoja na kuoneshan umma wanachoweza kufanya katika maendeleo ya taifa.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana aliwataka mafundi sanifu kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa lakini pia wawe waadilifu ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali kwa kiwango kilichokusudiwa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles