27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Erasto Nyoni awatoa hofu Watanzania

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

BEKI wa Taifa Stars, Erasto Nyoni, amesema atakinukisha katika mchezo wa pili wa timu hiyo dhidi ya Kenya wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon2019) inayoendelea nchini Misri.

Nyota huyo aliukosa mchezo wa juzi wa michuano hiyo, pale Stars ilipopokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa timu bora ya Afrika, Senegal, kwenye Uwanja wa June 30, jijini Cairo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Nyoni alisema alikuwa na maumivu hali iliyomfanya kocha wake, Emmanuel Amunike, ampumzishe.

“Nilikuwa na maumivu ndio maana sikuweza kucheza kwenye mchezo wetu dhidi ya Senegal, ila mchezo dhidi ya Kenya, nitakuwa nipo fiti na nitaonekana uwanjani,” alisema.

Alisema licha ya kufungwa, bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zinazowakabili mbele yao, hivyo watanzania waendelee kuwapa sapoti.

Taifa Stars itashuka tena dimbani Alhamisi kukabiliana na Kenya ‘Harambee Stars’, mchezo utakaopigwa kwenye dimba hilo la June 30 kuanzia saa 5:00 usiku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles