27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Emirates na Air Canada zaingia makubaliano ya ushirikiano

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shirika la ndege la Emirates na Air Canada zimeingia makubaliano ya pamoja za ushirikiano katika kuwapa fursa wateja wao nafasi mbalimbali za kuweza kupata manufaa ya mpango wa pamoja wa uaminifu wawapo safarini.

Makubaliano hayo yalitiwa saini hivi karibuni na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Idara ya Emirates Skywards, Dk. Nejib Ben Khedher na Makamu wa Rais Mwandamizi, Bidhaa, Masoko, Biashara ya Mtandaoni wa Air Canada na Rais, Aeroplan, Mark Youssef Nasr katika
Makao Makuu ya Emirates Group mjini Dubai.

Akizungumza katika makubaliano hayo, Khedher alisema watoa huduma hao waliamua kuanzisha ushirikiano huo wa kushiriki kwa lengo la kuwapa wateja muunganisho katika Bara la Amerika Kaskazini, Asia, Mashariki ya Kati na Afrika.

“Wateja wa Emirates sasa wanaweza kuhifadhi safari za ndege kwenda au kutoka maeneo ya Kanada hususani katika eneo la Toronto, ikijumuisha Calgary, Edmonton, Halifax, Montreal, Ottawa na Vancouver,”alisema na kuongeza:

“Tunafuraha sana kwa kuimarisha ushirikiano wetu na Air Canada na kuanzisha rasmi toleo letu la pamoja la uaminifu kwa pamoja, karibu wateja milioni 40 wanaosafiri wataweza usafiri kwa mtandao wa pamoja wa zaidi ya maeneo 350 na kufurahia huduma waliyochagua,”alisema Khedher.

Alisema wanatarajia kufungua fursa nyingine kwa wateja wao waaminifu na pia
kuwakaribisha wateja wa Aeroplan ndani ya Emirates na kuwaonyesha bidhaa zao zilizoshinda tuzo na huduma za kipekee.

Kwa upande wake, Nasr, alisema programu hizo mbili za makubaliano ni uaminifu
unaotambulika zaidi katika maeneo yao na zinakuja pamoja ili kutoa kitu kizuri katika usafiri wao was kutumia ndege hizo.

Alisema fursa hii itaweza kuunganisha marafiki na familia kutoka kwa watu wa Kanada na nchi nyingine na kusaidia wasafiri kuona baadhi ya maeneo yanayosisimua zaidi duniani.

“Tunajivunia kushirikiana na Emirates na Skywards huku Aeroplan ikiendelea kutimiza ahadi za Wateja wake kusafiri vizuri zaidi,makubaliano hayo mapya yatawawezesha wanachama wa Emirates Skywards kupata ya kutembea na kufanya safari zote za ndege za Air Canada zinazostahiki,”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles