25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

EMERY HATARINI KUFUKUZWA PSG

PARIS, Ufaransa


KOCHA wa Paris Saint Germain (PSG), Unai Emery, huenda akafukuzwa kazi muda wowote baada ya kushindwa kufikia matarajio ya mabosi wake ndani ya klabu hiyo.

Emery (46) ameendelea kusalia kwenye kibarua chake msimu huu licha ya kushindwa kutwaa taji la Ligue 1 na kupoteza kwenye kampeni za Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo Sport, viongozi wa PSG wamechoka kumvumilia, hata hivyo presha imezidi kuwa kubwa kwa kocha huyo wa zamani wa Sevilla dhidi yake na wachezaji wake.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa PSG wameshaanza kuandaa orodha ya makocha wanaoweza kutwaa mikoba ya Emery, akiwamo kocha wa Manchester United, Jose Mourinho na Mauricio Pochettino.

Lakini bado haijaeleweka kama kocha  huyo atavuka nusu ya msimu huu.PSG waliondolewa na Barcelona katika hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Februari  mwaka huu.

Matumizi makubwa ya fedha za usajili pia inawezekana kuwa chanzo cha presha kwa kocha huyo, baada ya kutumia pauni milioni 198 kumsajili Neymar Jr akitokea Barcelona na kukifanya kikosi cha Emery kuwa cha gharama zaidi duniani.

Ingawa PSG haijafungwa hadi sasa katika michezo 17, huku wakiwaacha kwa pointi nne wapinzani wao Monaco, lakini kocha huyo amedaiwa kuwa na uhusiano mbaya na baadhi ya wachezaji wake nyota.

Mkataba wa Emery ambaye anapokea pauni milioni tano kwa mwaka, unatarajia kumalizika Mei mwaka 2021 hivyo PSG watalazimika kumlipa dau nono ili kuvunja mkataba huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles