23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Emanuel awakumbuka wazazi na ‘Asante’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BAADA ya kimya cha muda mrefu, Mwimbaji wa Injili anayefanya kazi zake nchini Marekani, Emanuel Rashidi anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaoitwa, Asante Novemba 15, mwaka huu.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Emanuel amesema wimbo huo ni wa shukrani kwa wazazi jinsi walivyopambana katika malezi mpaka watoto wamefanikiwa kwenye maisha.

“Hatuna budi kusema Asante kwa wazazi wetu, Mungu aendelee kuwalinda. Huu wimbo unawahusu zaidi wazazi maana wametuzaa, wametutunza mpaka tumekuwa watu wazima sio jambo dogo.

“Hivyo, nitaachia audio na video hivyo mashabiki wa muziki wangu wakae mkao w akula kwa kufuatilia chaneli yangu ya youtube ili pale nitakapoachia kazi yangu basi wawe wa kwanza kuitazama,” amesema Emanuel Rashidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles