25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

EAC yajitoa kukabii corona kwa nchi wanachama

TEL AVIV, Israel

SEKRETARIETI ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imechukua uamuzi wa kuongeza juhudi dhidi ya kuenea kwa virusi vya corona (Covid-19) kwa kupeleka maabara zinazotembea na vifaa vya upimaji katika nchi zote washirika, baada ya mkutano maalumu wa mawaziri wa afya wa jumuita hiyo kukutana kujadili juu ya janga hilo.

Baraza la Mawaziri wa Afya lilifanya mkutano wake maalumu wa dharura kwa njia ya video ili kuharakisha mikakati ya haraka haraka kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo hatari unaosababisha vifo kwa wingi duniani kwa sasa, ambao tayari umeshaingia katika nchi zote wanachama wa EAC.

Mkutano huo unakuja wakati kesi za COVID-19 zikiwa zimeshathibitishwa katika nchi nne wanachama wa EAC kati ya sita, huku nchi zilizoathirika zikiendeela kuchukua hatua za kushughulikia tatizo hilo kwa kiwango cha kitaifa.

Rwanda ilikuwa nchi iliyoguswa zaidi katika Afrika Mashariki baada ya kuripoti kesi 36, ikifuatiwa na Kenya (kesi 15), Tanzania (kesi 12) na Uganda kesi tisa. Burundi a Sudan kusini badio hazijatoa taarifa kuhusu kuwepo kwa waathiriwa katika nchi zao.

Uganda ilikuwa imeripoti kesi moja tu hadi Jumatatu wiki hii lakini baada ya sampuli 35 kupimwa, watu wanane walithibitishwa kuwa na amambukizi.

Kesi zote nane ni raia wa Uganda ambao walirudi kutoka Dubai, Falme za Kiarabu; Wawili mnamo Machi 20 na sita mnamo Machi 22 ndani ya ndege za mashirika ya ndege ya Emirates na Ethiopia.

Ofisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Umma katika Idara ya Mawasiliano na Masuala ya Umma na Sekretarieti ya EAC, Peter Owaka alisema katika Makao makuu ya EAC Arusha kwamba kila nchi mwanachama itapatiwa gari maalumu kwa ajilim ya kuzungukakila sehemu kufanya vipimo vya maambukizi hayo.

Alisema magari hayo yana vifaa vyote muhimu vya maabara na ICT, na vile vile matumizi yote ya lazima kwa maabara inayofanya kazi kikamilifu na uwezo wa kufanya vipimo kwa ebola na virusi vya corona pamoja na virutubishi vingine.

Sekretarieti ya EAC pia imeweka Kamati ya Uratibu ya Kikanda (RCC) na Mawasiliano ya Dharura na ushiriki wa jamii; Sera na Miongozo; Fedha na vifaa na Kamati ndogo za Takwimu na Data na Takwimu kwa ajili ya usimamia majibu ya Covid-19.

Kamati ya Uratibu ya Kanda tayari imeanzisha shughuli kadhaa za kusimamia usalama kwa vyombo nataasisi za EAC, na kusaidia nchi washirika katika kupambana na virusi hivyo.

Juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo hatari kwa chombo hicho cha kikanda zinakuja wakati kila mmoja wa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anachukua hatua kupambana na janga hili.

Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda, Sudani Kusini na Burundi zimesimamisha ndege za kimataifa na Burundi ikienda maili zaidi kwa kusimamisha hata ndege za nyumbani.

G20 wafanya mkutano kwa njia ya vidio

Viongozi wa nchi zilizoendelea kiviwanda na zinazoinukia kiuchumi, G20 pia wamefanya mkutano kwa njia ya video jana, kuzungumzia mbinu za kupambana na mlipuko wa virusi vya corona, na kushughulikia matatizo ya kiuchumi yanayotokana na mripuko huo.

Mkuu wa Shirika la Afya Ulimenguni (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus pia alitoa ujumbe katika mazungumzo hayo, ambapo aliomba msaada wa kuwezesha utengenezwaji wa vifaa vya kujilinda dhidi ya maambuki ya virusi vya corona, ambavyo vimeadimika.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana mjini Geneva, Ghebreyesus alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa, katika kupambana na janga la virusi hivyo.

Virusi hivyo vimekwishawaua watu zaidi ya 21,000 miongoni mwa 471,000 waliokwishaambukizwa kote duniani.

Mapema wiki hii, mawaziri wa fedha na wakuu wa benki kuu kutoka nchi hizo, waliweka mkakati wa kudhibiti virusi hivyo, lakini hawakutoa maelezo zaidi.

Hispania yavunja rekodi

Kwa mujibu wa BBC, Hispania sasa limekuwa taifa la pili kuongoza kuwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya corona duniani.

Idadi ya vifo imeongezeka kwa watu 738 ndani ya saa 24 kila siku na kufanya idadi ya vifo hivyo mpaka sasa kufikia 3,434, idadi ambayo iko juu zaidi ya Italia.

Ukilinganisha taarifa rasmi za China ambazo ziliripoti vifo 3,285 huku nchi ambayo imeathirika zaidi duniani, Italia ikiwa na vifo 6,820.

Idadi ya maambukizi Hispania imeongezeka mara tano na karibu watu 27,000 wanatibiwa kila siku hospitalini.

Pamoja na mazuio mengi duniani bado virusi vya corona vinaonekana kuwa changamoto kubwa duniani.

Wakati huohuo Marekani ikiwa kwenye hali tete ambapo visa 70,000 vya virusi vya corona vimethibitishwa na vifo vyapatavyo 1,050 .

Idadi ya maambukizi imeonekana kuongezeka kwa zaidi ya 10,000 kwa siku moja.

Kwa upande wa Uingereza vifo vimeongezeka na kufikia 463, awali vilikuwa 422, wakati maambukizi ya ugonjwa huo yakiwa zaidi ya 9,500.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles