27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wasaudi 20 washtakiwa kwa mauaji ya Kashogi

ANKARA, UTURUKI

UTURUKI imewashtaki raia 20 wa Saudi Arabia wanaotuhumiwa kumuua mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, akiwemo aliyekuwa naibu mkuu wa kitengo cha ujasusi, mshauri wa familia hiyo ya kifalme pamoja na washukiwa wengine 18.

Kupitia taarifa yake, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka mjini Istanbul imesema imekamilisha uchunguzi wa mauaji ya mwandishi huyo wa habari aliyeuawa katika Ubalozi wa Saudia mjini Istanbul mwaka 2018.

Mauaji hayo yalilaaniwa vikali kote duniani na hivyo kulipaka tope jina la mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia Arabia, Mohammed bin Salman.

Baadhi ya Serikali za Magharibi kikiwemo pia kitengo cha ujasusi cha Marekani (CIA), kilimnyooshea kidole cha lawama Mohammed bin Salman wakimtuhumu kuwa aliagiza mauaji ya mwandishi huyo, tuhuma ambazo Saudia zimekanusha.

Hata hivyo, washukiwa wote wa mauaji hayo tayari wameondoka Uturuki na Saudi Arabia imekataa wito wa Uturuki wa kuwarudisha nchini humo ili wahukumiwe.

Badala yake Saudia inasisitiza kuwa mahakama zake zina uwezo wa kuendelea na kesi hiyo.

Tayari watu 11 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya Khashoggi wamepandishwa kizimbani nchini Saudia Arabia.

Kupitia taarifa yake, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka mjini Istanbul inayoongozwa na Irfan Fidan alisema kuwa Ahmed Al Asiri na Saud al Qahtani walikuwa na nia mbaya iliyolenga kushawishi mauaji ya Mwandishi huyo wa Habari ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa Ufalme wa Saudia.

Ofisi hiyo vile vile ilisema kuwa inawatuhumu watu wengine 18 kwa kuhusika na mauaji ya Khashoggi akiwemo raia mmoja wa Marekani na mwandishi katika gazeti la Washington Post na inapendekeza kifungo cha maisha gerezani kwa watuhumiwa hao.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa mashtaka dhidi ya washukiwa hao yalitokana na uchunguzi wa rekodi zao za simu, safari zao za kuingia na kutoka Uturuki, uwepo wao katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul, taarifa za mashahidi pamoja na uchunguzi wa kompyuta na simu ya Khashoggi.

Khashoggi ambaye alikuwa akiishi Marekani, alikwenda katika Ubalozi wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2, 2018 kwa ajili ya kuchukua nyaraka ambazo zingemuwezesha kufunga ndoa na mchumba wake raia wa Uturuki.

Hata hivyo, baada ya kuingia ndani ya Ubalozi huo hakutoka tena na hadi leo mwili wake haujapatikana.

Timu ya watu 15 kutoka Saudia ambao wanawajibika moja kwa moja kwa bin Salman walisafiri hadi Uturuki kukutana na Khashoggi ndani ya Ubalozi huo.

Maofisa wa Uturuki wanadai kuwa Khashoggi aliuawa ndani ya Ubalozi huo na kisha mwili wake ukakatwa vipande vipande.

Haya yanajiri baada ya mahakama ya Saudia kuwahukumu kifo watu watano na wengine watatu kupewa kifungo cha gerezani tangu Disemba, kwa kuhusika na mauaji ya Khashoggi lakini mwendesha mashtaka wa Saudia alisema hakuna ushahidi wowote wa kuwahusisha Qahtani au Asiri na mauaji hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles