27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Dully: Walioshindwa kumzika baba yangu wamenihuzunisha

ebbyNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, ameshangazwa na kitendo cha wasanii wengi kutojitokeza katika mazishi ya baba yake mzazi, Ebby Sykes juzi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini juzi mara baada ya kumalizika kwa mazishi ya baba yake, msanii huyo alisema ameshangaa jinsi gani wasanii wengi wamekuwa na roho za chuki.
Alisema matarajio yake yalikuwa kuwaona wenzake wakiungana naye katika wakati huo mgumu, lakini ni wachache sana walioonyesha moyo wa upendo na ukaribu.
“Nilitegemea kwakuwa tunampumzisha baba yangu hapa hapa Dar es Salaam, wangekuja wasanii wengi ambao ni marafiki zangu, lakini hali ilikuwa tofauti kabisa,” alisema.
“Sijui walijua nitakuja kuwaomba fedha zao, mimi nilishapata michango mingi kutoka kwa watu wengine mbalimbali, ukweli wasanii tuache roho za kimasikini,” alisema.
Sykes aliendelea kusema amegundua asilimia kubwa ya wasanii wamekuwa wakipendana wakati wa raha tu, lakini inapofika muda wa matatizo kila mmoja hukimbia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles