30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

DStv yawakutanisha mastaa visiwa vya Mauritius

dstv Genevieve-Ramsey-Noah-at-October-1st-movie-premiere-HouseOfmaQNA SELEMAN SHINENI, MAURITIUS

MASTAA mbalimbali wanaojishughulisha na masuala ya burudani kutoka barani Afrika, waandishi wa habari na watu mashuhuri wamekutanishwa katika visiwa vya Mauritius kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa Tamasha la 2015 Content Showcase Extravaganza.

Hafla hiyo ilifanyika juzi kwenye hoteli ya Outrigger Resort ikiwa ni mwanzo wa tamasha hilo la wiki moja lililoandaliwa na Kampuni ya MultiChoice Africa huku dhumuni lake kuu likiwa ni kuonyesha maudhui yaliyopo kwenye ving’amuzi vya DStv.

Baadhi ya mastaa waliokutanishwa katika tamasha hilo lililoandaliwa na Kampuni ya MultiChoice Africa ni Genevieve Nnaji, Ramsey Nuoah, Rita Dominic na Desmond Elliot ambao ni waigizaji mashuhuri nchini Nigeria.

Wengine ni wasanii wa muziki Mr Flavour na Stonebwoy kutoka kundi la The Mavin ambao walitumbuiza katika tamasha hilo kwa nyimbo zao mwanana.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Tim Jacobs, alisema kampuni yake imejipanga kuongeza burudani zaidi karibu na wateja wao ili wateja wao wapate kila kitu kupitia DStv.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles