23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Dream teams zaelekea Dodoma

Sharifa Mmasi, Mtanzania Digital

TIMU za mpira wa kikapu za Dar es Salaam ‘Dream teams’, zimeondoka leo Novemba 4, 2021 kuelekea Dodoma kwa mashindano ya Taifa,  ‘CRDB Taifa Cup’ yanayoanza kesho Ijumaa jijini humo.

Kocha Mkuu wa timu hizo, Asharf Haroon, amesema vikosi vyote viwili yaani timu ya wanaume na wanawake zipo katika morali za hali ya juu kwenda kuchuana na kurudi nyumbani na ubingwa.

Amesema kupitia mashindano hayo msimu uliopita timu yao ya wanawake iliibuka kidedea huku wanaume wakimaliza nafasi ya pili hivyo, watahakikisha wanakwenda kutetea ubingwa huo kwa kuchukuwa makombe mawili dhidi ya mikoa pinzani.

“Tupo safarini kuelekea jijini Dodoma kushiriki mashindano ya CRDB Taifa Cup ambayo yataanza rasmi kesho Ijumaa, kwa upande wa timu zote mbili za Mkoa wa Dar  es Salaam, wachezaji wote wapo katika morali ya hali ya juu lakini kubwa niseme tunakwenda kupambana na tutarudi nyumbani na ushindi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles