24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

DRC yaomba msaada wa upatanishi

KINSHASA, DRC

SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imemuomba Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe apatanishe katika mgogoro wa mpaka baina yake na Zambia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC, Marie Tumba Nzeza, ambaye pia ni mjumbe maalumu wa rais wa nchi hiyo amekutana na Rais Mnangagwa katika Ikulu mjini Harare na kumfahamisha kuhusu mgogoro huo.

Rais Mnangagwa aliombwa apatanishe katika mgogoro huo kama  mwenyekiti wa sasa wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc).

Baada ya mkutano huo, Rais Mnangagwa alisema nchi hizo mbili zinataka Sadc isuluhishe mgogoro huo.

Zambia na DRC zinahitilafiana kuhusu mpaka wao wa pamoja wenye urefu wa kilomita 1,600 ambapo mvuntano unahusu sehemu unakoishia mpaka huo.

Hii si mara ya kwanza kwa Sadc kutakiwa kutatua mgogoro wa mpakani baina ya nchi wanachama. 

Katika muongo wa miaka ya 1990, Sadc ilijaribu kupatanisha bila mafanikio mgogoro wa mpakani baina ya Botswana na Namibia kuhusu umiliki wa kisiwa katika Mto Chobe ambao uko katika mpaka wa nchi hizo mbili.

Kesi hiyo hatimaye ilifikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ambayo mwaka 1999 ilisema kisiwa hicho ni milki ya Botswana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles