26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

DRC imeahirisha chanjo dhidi ya Covid-19

DR, Kongo

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeamua kuahirisha chanjo dhidi ya covid-19, Operesheni ya kutoa chanjo hiyo ilikuwa imepangwa kuanza leo Jumatatu, lakini kulingana na taarifa ya Wizara ya Afya ya nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,zoezi hilo litafanyika tu baada ya uchunguzi juu ya athari za chanjo ya Astra Zeneca kukamilika.

Ni zaidi ya wiki moja tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupokea dozi zaidi ya milioni moja na laki Saba na hivyo kuwa moja ya nchi za kwanza barani Afrika kupokea chanjo hizo zilizoidhinishwa na kusafirishwa chini ya mpango wa COVAX. Lakini kwa tahadhari, viongozi wa Kongo wameamua kuahirisha uanzishaji wa kampeni ya chanjo hiyo, kama ilivyofanywa na baadhi ya nchi za Ulaya kutokana na ripoti kwamba watu waliopewa chanjo hizo wanapata matatizo ya kuganda damu.

Mjini Kinshasa unasubiriwa uthibitisho kutokana na madai hayo, kama anavyoeleza Daktari Eteni Longondo, Waziri wa Afya wa Kongo, ambaye anasisitiza umuhimu wa chanjo hiyo anasema “Chanjo ndio njia bora zaidi kwa kumaliza janga. Tunasubiri kuhitimishwa kwa utafiti unaoendeshwa na Wazungu, pia ule wa kamati yetu ya kisayansi hapa nyumbani ili kuchukuwa hatua ya mwisho. Ila kwa sasa, tumesitisha,” alisema waziri huyo.

Hatua hiyo ya serikali ya Kongo imechukuliwa baada ya mbunge Bertin Mubonzi kutoka chama cha UNC kumuuliza Waziri wa afya swali la usalama wa chanjo hiyo. Bertin Mubonzi sasa ameridhishwa na hatua hiyo, akisisitiza kwamba ni faida ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  kuzingatia kinachoendelea katika nchi nyingine, ili kuwakinga raia wa Kongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles