24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

DPP amng’ang’ania Kitilya, wenzake

DPPNA MANENO SELANYIKA, DAR ES SALAAM

MKURUGENZI wa Mashtaka  (DPP), Biswalo Mganga amewasilisha kusudio la kukata rufaa ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Saalam, ya kutupilia mbali rufaa iliyowasilishwa mahakamani hapo katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili.

Kusudio hilo liliwasilishwa Mei 6 mwaka huu katika Mahakama hiyo baada ya Jaji Mfawidhi, Mosses Mzuna kusema kuwa hoja zilizowasilishwa na mawakili wa Jamhuri katika rufaa hiyo hazikuwa na msingi.

Wiki iliyopita Mahakama Kuu ilitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na DPP ya kupinga uamuzi wa kufutwa  shtaka la nane linalowakabili washtakiwa hao kwa madai kuwa hoja zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri hazina msingi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni   aliyekuwa MissTanzania (1996), Shose Sinare na Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tawi la Tanzania, Sioi Solomon.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kutakatisha Dola za Marekani milioni sita kwa kuzihamisha kutoka katika akaunti ya Kampuni ya Egma.

Hata hivyo, Aprili 27, mwaka huu, Mahakama ya Kisutu iliwafutia shitaka hilo na kubakiwa na mengine ambayo yanadhaminika baada ya upande wa utetezi kuiomba mahakama iliondoe kwa madai kuwa halijakidhi vigezo vya sheria kwa kuwa hakuna maelezo ya wazi jinsi walivyotenda kosa hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles