Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
MBUNGE wa Ukonga, Jerry Slaa amesema hatua ya Serikali kutafuta mwekezaji kwenye Bandari nchini itasaidia kuongeza mapato na kuinua sekta ya Bandari.
Slaa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ameyasema hayo leo Julai 12, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa Serikali kutaka kuingia makubaliano ya uwekezaji na kampuni ya DP World ya Dubai.
Aidha, Slaa amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan haikukurupuka kutafuta mwekezaji wa bandari lengo lake lilikuwa ni kuboresha sekta ya hiyo kwa kuongeza ufasini na kuchangia mapato ya Serikali.
Hata hivyo, Slaa amepinga kwa wale ambao wanadai wananchi hawakutoa maoni na kufanya kuwa Bunge kupitia Kamati yake ya PIC walipokea maoni kwa wananchi na kufikia bunge hatua ya kupitisha uwekezaji huo.