25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Dortmund yambania Aubameyang kuondoka

Pierre-Emerick-AubameyangDORTMUND, UJERUMANI

KLABU ya Borrussia Dortmund ya nchini Ujerumani, imedai kwamba mshambuliaji wake, Pierre Aubameyang, hawawezi kumwachia akajiunga na klabu nyingine kwa sasa.

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Gabon, ambaye amechukua uchezaji bora wa Afrika (CAF) kwa mwaka 2015, amekuwa akiwindwa na klabu mbalimbali katika kipindi hiki cha usajili, lakini uongozi wa klabu hiyo umedai kwamba hauna mpango wa kumwachia mchezaji huyo kuondoka.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa klabu hiyo, Hans Watzke, amesisitiza kwamba wachezaji wao wote watawazuia kuuzwa katika kipindi hiki cha usajili wa Januari akiwemo Aubameyang ambaye anawaniwa na klabu ya Arsenal.

“Hatuwezi kuwaachia nyota wetu kwa sasa katika kipindi hiki cha dirisha la usajili Januari, tunajua kwamba kuna klabu nyingi kwa sasa zinawaangalia wachezaji wetu ambao wanafanya vizuri.

“Hatupo tayari kuwaachia waondoke, bado tunahitaji mchango wao ili kuweza kuipa heshima klabu yetu,” alisema Watzke.

Aubameyang amekuwa ni mchezaji ambaye anaangaliwa sana na klabu mbalimbali kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa hasa katika kupachika mabao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles