Na RAMADHAN HASSAN -D0DOMA
SERIKALI imewataka wawekezaji nchini kuchangamkia fursa ya ujenzi wa hoteli zenye nyota nne ama tano kutokana na kutokuwepo mkoani humo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Serikali kuzitangaza hoteli tatu pekee zenye nyota tatu mkoani hapa ambazo ni Fantacy Village, Nashera Hoteli na New Dodoma Hoteli.
Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu, wakati wa hafla ya kutoa daraja za nyota kwa hoteli zi- lizopangwa katika daraja za ubora jijini Dodoma.
Kanyasu alisema licha ya Jiji la Dodoma kuwa ndio makao makuu ya Serikali, bado kuna mahitaji ya hoteli zenye nyota nne na tano hivyo akawa- taka wawekezaji kuchangamkia fursa hiyo kwa kujenga hoteli zenye ubora.
“Wito wangu hatuna hoteli zenye nyota nne na tano hapa Dodoma, ni- waombe wawekezaji kuchangamkia fursa hii, kutafuta maeneo kwani Jiji la Dodoma linatoa na maeneo hayo yapo,”alisema.
Alisema kuwepo kwa hoteli nzuri kutachangia kuwafanya watalii am- bao huja nchini kufikia katika maeneo yenye ubora hivyo kuliongezea taifa mapato.
“Hitaji la wageni ni malazi na huduma bora hivyo upangaji wa madaraja ni jambo muhimu, wito wangu kwa wamiliki wa hoteli kuwa na lugha nzuri kwa wageni ambao wanawapokea,”alisema.
Aidha alisema changamoto am- bazo wamekuwa wakikutana nazo ni hoteli kujengwa sehemu ambazo sio sahihi na kuwepo kwa wafanyakazi ambao hawana sifa.
“Niwaombe wamiliki wa hoteli ambazo tumezikagua na kukuta hazi- jakidhi vigezo kuliangalia kwa uma- kini jambo hili kwa kujenga sehemu sahihi na kuchagua wafanyakazi we- nye sifa,”alisema.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pro- fesa Adolf Mkenda, alisema zoezi la kupanga madaraja ya nyota kwa holeli lilianza katika mikoa ya Dar es salaa, Pwani, Arusha, Mara na sasa Dodoma.
Alisema lengo la zoezi hilo ni kubaini ubora wa hoteli ili kuwasaidia Watanzania na wageni ambao wana- toka nje ya Tanzania kujua ni sehemu gani wanatakiwa kufikia pindi wa- napokuja nchini na kujua ubora wa hoteli.
Alisema wameanzisha mfumo wa kieletroniki ambao utakuwa uki- wawezesha wamiliki wa hoteli kupi- ma ubora wa hoteli zao.
Katibu Mkuu huyo alisema kwa Mkoa wa Dodoma walikagua, hoteli, nyumba za wageni 428 ambapo wal- izokuta zina ubora ni 24 pekee.
Naye mfanyatathmini kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Hassan Rehani, alisema wamekuwa wakitoa nyota za hoteli kutokana na kujaza madodoso ambayo baadaye huangalia ubora, pamoja na kutumia vigezo tisa ikiwemo kuwepo kwa vifaa vya kuzuia majanga.