23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru yadaka doti 600 za vitenge vya CCM

Na GRACE SHITUNDU -DAR ES SALAAM

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Shinyanga imekamata doti 600 za vitenge vyenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nyumbani kwa Joseph Tasia ambavyo vimetiliwa shaka kutumika kama rushwa katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa umma Mkuu wa Takukuru Shinyanga, Hussein Mussa alisema ukamataji wa doti hizo ulifanyika Juni 29 mwaka huu Mtaa wa Mwasele B Shinyanga.

“Juni 29 mwaka huu saa tatu usiku mtaa wa Mwasele B nyumbani kwa Joseph Jonas Tasia zilikamatwa doti 600 za vitenge vyenye nembo ya CCM na vya kawaida vikiwa

vimehifadhiwa nyumbani kwake jambo ambalo linaashiria vilikuwa vinaandaliwa kutumia katika kufanya ushawishi kwa wapiga kura”, alisema Mussa.

Alisema katika mahojiano yaliyofanywa na maofisa wa Takukuru, mtuhumiwa alishindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza kuhusiana na mzigo uliokutwa nyumbani kwake na pia nyaraka za manunuzi ya mzigo huo hazijitoshelezi na kuongeza shaka juu ya uhalali wa vitenge hivyo.

“Aidha uchunguzi wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga umebaini kwamba Tasia ambaye ni mfanyabiashara wa usafiri wa magari madogo Taxi hana duka na wala hafanyi biashara ya kuuza vitenge”, alisema Mussa.

Mkuu huyo wa Takukuru

Shinyanga alisema kuwa hata hivyo uchunguzi wa kina bado unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli na taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguzi huo.

“Uchunguzi wa kina bado unaendelea ili kubaini iwapo vitenge hivyo vilikuwa ni kwa ajili ya kuhusika na vitendo vya rushwa katika uchaguzi ujao au ni kwa ajili ya kufanya biashara katika msimu huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa viongozi.

Alisema taasisi hiyo imewaonya watu wote wenye nia ya kutaka kutumia taarifa zozote za uchunguzi zinazofanyiwa kazi na ofisi hiyo kwa nia ya kujinufanisha kisiasa na kwamba kitendo hicho ni kuingilia uchunguzi unaondelea na ni kosa la jinai hivyo atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles