24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Sita mbaroni kwa kuchinja watu wanne Kahama

Na SAIMON MHENDI -KAHAMA

KAIMU Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paulo, amese- ma watu sita wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyofanyika Segese Msalala wilayani Kahama Mkoa wa Shin- yanga.

Katika mauaji hayo, watu wa- naodhaniwa kuwa ni majambazi walichinja watu wanne na kumje- ruhi mmoja.

Majambazi hao wanadaiwa kutekeleza tukio hilo la Juni 30 ka- tika maeneo ya kiwanda cha uchen- juaji dhahabu katika Kijiji cha Wi- solele na ambapo waliiba carbon na kutokomea.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Segese, Evagisla John, alisema ma-

jambazi hao walifanya tukio hilo saa tisa alfajiri.

Alisema waliouawa ni mtu aliye- julikana kwa jina la Danieli, Raphaeli Kipea ambaye alikua ni msimamizi katika planti hiyo na walinzi wawili ambao ni Lusajo Marko alietambu- liwa kwa jina moja pamoja na Juma.

Alimtaja mtu aliyejeruhiwa kuwa ni Hashimu ambaye anaende- lea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya Kahama.

“majambazi walivamia katika planti wakaiba carbon zilizokua mle, wakauwa watu wanne na kujerui moja na jambo hili lipo polisi uchun- guzi unaendela,”alisema John.

Kutokana na tukio hilo, baadhi ya wananchi wameomba kujengwa kituo cha polisi kijiji hapo ili kuweza kuondoa vitendo hivyo vya uhalifu.

“Kusema ukweli hali ya ki-

usalama hapa imekua ni ngumu, watu tumekua na hofu tunashind- wa kufanya kazi zetu kwa uhuru, eneo hili linakusanya watu wengi sasa kiusalama hali inakua mbaya, niwaombe Serekali iliangalie hili” alisema Aliphonce Antoni ambae ni mchimbaji mdogo katika eneo hilo.

Naye John Tungaraza alisema mauaji hayo ya kikatili yamefanya watu wengi katika kijiji hicho ku- ingiwa na hofu, na kutoa kilio chake kwa Serekali akiomba kujengwe kit- uo cha polisi katika machimbo hayo.

“Inasikitisha sana kwa tukio la watu wa nne kuuwawa kikatili nam- na hii, mimi sijawahi kuona niliwahi kusikia watu wanavamiwa kwenye mabasi na majambazi na kuporwa lakini si kwa staili hii, kwa ukweli imenizunisha sana” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,249FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles