26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Slaa: Simba, Yanga bure kabisa

3

NA EZEKIEL TENDWA
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilbroad Slaa, amezitolea uvivu klabu za Simba na Yanga kusema hazina jipya.
Slaa alitoa kauli hiyo juzi Jumapili kwenye mkutano wa kumpongeza mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kibwegere, Edson Nyingi, uliofanyika kwenye viwanja vya Makombe, Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo, Dk. Slaa alisema kwa sababu Simba na Yanga zimeshindwa kufika popote, ni lazima zitafutwe timu mbadala za kuweza kuchukua nafasi zao.
Alisema anasikitishwa na klabu hizo kwani licha ya ukongwe zilionao katika Soka la Tanzania zimeshindwa kuitangaza nchi kimataifa.
“Sina ugomvi na Simba wala Yanga, lakini lazima tukubaliane kuwa zimeshindwa kuitangaza nchi kimataifa na hii ni kutokana na mipango mibovu ya klabu hizi, hivyo ni wakati wa vijana kujipanga kuanzisha timu zenye malengo.
“Angalia Azam, licha ya kwamba ni timu changa iliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni, lakini imeonyesha dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo ya soka kama tunavyoshuhudia tayari wana uwanja wao,” alisema Dk. Slaa.
“Wana vitendea kazi vingi na wapo wanazingatia soka la vijana lakini Simba na Yanga ziko pale pale miaka nenda rudi, ni dhahiri kwa mwenendo huu hawatafika.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles