25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Dk. Shein amwapisha Balozi Idd

DSC_2021Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, jana alimwapisha  Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Dk. Shein alimteua Balozi Iddi kushika wadhifa huo, wiki iliyopita kwa mujibu wa kifungu cha 39(2) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

Uteuzi wa Balozi Iddi ni uteuzi wa pili wa kufanywa na Rais Dk. Shein tangu alipoapishwa Alhamisi iliyopita kuanza kipindi chake cha pili.

Sherehe hizo, zilifanyika Ikulu Zanzibar zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakiongozwa na  Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu, Said Hassan Said.

Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu Sheikh Omar Kabi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghribi, Abdallah Mwinyi Khamis na Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Khatib Abdulrahman Khatib.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles