23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Meya: Nataka kujua mali,mikataba ya Jiji

MEYA ISAYA MWITAAsifiwe George na Johanes Respichius, Dar es Salaam

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya  Mwita amesema anataka kujua mali na mikataba yote iliyoingiwa ili ajipange kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa jiji hilo.

Meya Mwita, ametoa kauli hiyo Dar es Salaam jana, baada ya kuapishwa na Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa Mahakama  ya Sokoine Drive, Aziza Kali mbele ya Mkurugenzi wa jiji hilo, Wilson Kabwe.

“Jiji letu kwa muda mrefu lilikuwa halina meya, natamani kujua mali za wananchi ziko wapi na kuangalia namna ya kuwasaidia wamachinga, mama lishe na waendesha bodaboda,” alisema.

Alisema atashirikiana na watendaji wote ili  kuhakikisha wanatoa huduma za jamii, kuhamasisha suala la usafi, kupunguza foleni katika jiji hilo.

Alisema anasikitishwa na huduma duni za elimu, hasa suala la upatikanaji wa madawati ambapo hadi sasa baadhi ya shule wanafunzi wanakaa chini.

“Sula la wanafunzi kukaa chini  katika halmashauri yenye kukusanya  mapato makubwa ni aibu, nawaomba wafanyabiashara wote kuzingatia ulipaji wa kodi ili fedha hizi zisaidie shughuli nyingine za maendeleo, ikiwamo kutengeneza madawati, upatikanaji wa dawa na kukarabati barabara katika mitaa yetu.

“Tunakabiliwa na changamoto ya kuhifadhia takataka (dampo), kuna eneo moja, nitahakikisha kila wilaya inakuwa na dampo na yatakuwapo Kinondoni, Temeke, Kigamboni na Ubungo,” alisema .

Alisema kila kata vijana wametengewa Sh milioni 200 ambapo utekelezaji wake umeanza Wilaya ya Kinondoni kwa vijana kutakiwa kuunda vikundi kwa ajili ya kupata mikopo.

Kuhusu suala la bomoabomoa ambalo lilifanyika  eneo la Mkwajuni, Matata alisema hakubaliani nalo kwani ni kuwaumiza wananchi.

Sherehe za kuapishwa Meya Matata zilihudhuriwa na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), Meya wa Ilala, Charles Kuyeko  na wafuasi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles