25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Nawanda: Bingwa Simiyu Super Cup atavuna mamilioni

Na Samwel Mwanga, Simiyu

MKUU Wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahaya Nawanda amesema kuwa bingwa wa Michuano ya soka ya Simiyu Super Cup 2023 anatarajia kubeba kitita cha Sh milioni Nne.

Akizindua mashindano hayo na kuzungumza na viongozi wa vilabu ya soka na wa vyama vya soka vya wilaya zote za mkoa huo katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Nawanda amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuwaunganisha vijana, kuleta umoja na mshikamano kwa vijana wa mkoa wa Simiyu kupitia mashindano ya Mpira wa miguu.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dk. Yahaya Nawanda(wa nne kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama na Viongozi wa Chama Cha Mpira wa miguu Mkoa wa Simiyu baada ya kuzindua mashindano ya Simiyu Super Cup 2023 mjini Bariadi.

Amesema kuwa mashindano hayo yatachezwa kuanzia ngazi ya Wilaya na bingwa wa kila wilaya ataungana na timu nne kutoka wilaya ya Bariadi katika hatua ya robo fainali hadi fainali na michezo hiyo itafanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi.

Dk. Nawanda amesema kuwa atatoa jezi seti Moja na Mpira mmoja mmoja kwa kila timu itakayoshiriki hatua za Awali za mashindano hayo pia na kwa timu zitakazoingia hatua ya robo fainali pia zitapewa tena seti moja ya jezi kwani anazo jezi za kutosha

“Mshindi wa kwanza kwenye mashindano haya atampata zawadi ya Sh milioni Nne, mshindi wa pili Sh milioni tatu na mshindi wa tatu Sh milioni moja.

“Tunagawa jezi seti moja na mpira mmoja kwa kila timu katika hatua hii ya awali na hatua ya robo fainali pia tutatoa jezi seti moja kwa kila timu kwa kuwa tunazo jezi za kutosha,”amesema Dk. Nawanda.

Amesema mashindano yote hayo yataratibiwa na Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Simiyu (SIFA) huku akiwaagiza Wakuu wa Wilaya zote za mkoani humo kuwa walezi wa timu zinazoshitiki mashindano hayo kwenye wilaya zao.

Aidha, amesema kauli mbinu ya mashindano hayo itakuwa “Tumekiwasha,Tumekufikia,twende pamoja na Mama Samia”.

Naye Mwenyekiti wa SIFA, Osuri Kosuri amesema kilichofanywa na Dk Nawanda hakijawahi kufanywa na kiongozi yeyote wa Serikali mkoani humo tangu uanzishwe na kuhakikisha kuwa watayasimamia kwa kufuata kanuni zote 17 za mchezo wa mpira wa miguu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles