26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwinyi mgeni rasmi mashindano ya Quran

Brighiter Masaki

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya 21 ya Quran Tukufu ya Afrika yatakayofanyika Aprili 25,2021 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Aidha, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgenimashuhuri kwenye mashindano hayo yatakayoshirikisha nchi 21.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Machi 30, jijini Dar es Salaam, Shekh Nurdin Kishki amesema kuwa mshindi wa kwanza atapata nyumba yenye vyumba vinne na flemu za biashara iliyoko Temeke.

Amefafanua kuwa iwapo mshindi atatokea nchi nyingine amesema:

“Iwapo mshindi akitokea nchi nyingine atapata kiasi cha Sh milioni 20 kama Mtanzania atakabiziwa nyumba ambayo ipo Temeke.

“Mvua au jua isiwe sababu ya kukufanya kushindwa kushiriki mashindano haya na watakao shinda watapata zawadi,” amesema Sheikh Kishki.

Kwa Upande wake Katibu wa shindano hilo, Hussein Kiza amezitaja nchi zitakazoshiriki mashindano hayo kuwa ni pamoja na Uganda, Kenya, Burundi, Sudani, Congo, Senegal, Cameroon, Msumbiji, Nigeria, Nijar, Serilion na Benin.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles