25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwanjelwa aupa neno mtandao sera 

Na Mwandishi wetu,Mbeya

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa amesema uanzishwaji wa mtandao wa sera (Policy Network), utasaidia kuleta matokeo chanya juu

ya ushiriki wa wanawake katika sekta za kilimo,mifugo na uvuvi.

Akifungua mkutano wa siku moja  uliowakutanisha wadau kutoka Kongani za Ihemi na Mbarali katika Ukanda wa  Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu

Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) kwa lengo la kujadili, kutathmini na kukubali miongozo ya kazi ya mtandao wa sera, Dk. Mwanjelwa alisema mtandao huo utachochea ushikiriki wa wanawake katika sekta hizo muhimu.

“Nategemea kupitia mtandao wa sera utakuwa mkombozi  kutambua ushiriki wa wanawake na wanaume  katika sekta ya kilimo ili kuwe na usawa katika uzalishaji na kipato kwa wote,”alisisema.

Alisema nafasi kubwa ushiriki wa wanawake katika kilimo,inaonekana wakati wa maandalizi ya shamba,kulima na kuvuna lakini wakati wa mauzo huwekwa nyuma.

“Wito wangu kwa watendaji wa SAGCOT na wadau wake, ni kuandaa warsha na semina elekezi juu ya mtandao wa sera ili kujenga uwelewa katika ngazi

zote kwenye ukanda huu ili tija itakayopatikana huku, ikawe mwongozo katika maeneo mengine  hapa nchini,” alisema

Alisema hatua iliyochukuliwa na SAGCOT kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA) kufanya utafiti huu ambao umesaidia kuleta mapendekezo mbalimbali juu ya changamoto zilizopo katika ushiriki wa mwanamke katika sekta ya kilimo, ni wa kupongezwa.

Katika hatua nyingine, Dk.Mwanjelwa alikubali ombi lakuwa mlezi wa Mtandao Sera na kuwataka SAGCOT na wadau wake kutoa mrejesho wa utekelezaji wa sera hiyo kwa kila baada ya miezi mitatu ili kupima mafanikio yake.

“Nimekubali pendekezo lenu kwa kuwa swala yenyewe linaihusu wizara ninayoifanyia kazi na pia linamhusu mwanamke,”alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sera wa SAGCOT,Neema Lugangira alisema lengo kuu la kufanya warsha hiyo,  ni kutoa mrejesho wa tafiti

iliyofanywa na SAGCOT  kwa kushirikiana na TAWLA kutazamia changamoto zilizopo za ushiriki wa mwanamke katika sekta ya kilimo.

“Tunafanya miradi mingi ya maendeleo kupitia wadau wake mbalimbali hivyo tumeonelea ni vizuri kukawa na sera, itakayotupa mwongozo katika kumshirikisha mwanamke katika kilimo, mifugo na uvuvi ili kumwinua kiuchumi,” alisema Lugangira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles