24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

 Mabao ya Samatta yamwibua Zitto Kabwe

NA MOHAMED KASSARA, DAR ES SALAAM

MABAO mawili aliyofunga nahodha wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta, katika mchezo wa Ligi ya Europa, yamemfanya Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, kushindwa kuzuia hisia zake na kumpongeza akisema yameliletea heshima Taifa.

Samatta alifunga mabao hayo katika mchezo wa kundi I, Ligi ya Europa na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya vigogo wa Uturuki, Besiktas.

Mabao hayo yaliifanya timu hiyo kuongoza msimamo wa kundi baada ya kufikisha pointi sita katika michezo  mitatu, ikishinda miwili na kufungwa mmoja, ikifuatiwa na Malmo FF yenye pointi nne sawa na Sarpsborg 08, wakati Besiktas ina pointi tatu ikishika mkia.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Kabwe, alimpongeza mshambuliaji huyo kwa kiwango alichokionyesha katika mchezo huo na kufunga mabao hayo ambayo yameiletea heshima  kubwa Tanzania.

“Nianze kwa kumpongeza Samatta kutokana na kufunga mabao mawili michuano ya Europa, kwani mabao hayo yameliletea Taifa heshima kubwa,” alisema Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini.

Samatta amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu, ambapo hadi sasa ameshapachika mabao 10 katika michuano hiyo, akianza kufunga mabao saba katika michezo mitano, kabla ya kufunga mengine matatu katika hatua ya makundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles