24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Dk Msola Mwenyekiti mpya Yanga

ADAMU MKWEPU_DAR ES SALAAM

DK Mshindo Msola ameshinda kiti cha uenyekiti wa klabu ya Yanga, baada ya kupata kura 1376 dhidi ya 70 za mpinzani wake Dk Jonas Tiboroha, katika  uchaguzi uliofanyika Bwalo la Polisi Oyster bay, Dar es Salaam jana.

Msimamizi wa uchaguzi huo kutoka Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Malangwe Mchungahela akitangaza matokeo hayo, alisema jumla ya wanachama 1341 wa Yanga walipiga kura kumchagua mwenyekiti huku kura  tano kati ya hizo zikiharibika.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela aliibuka kidedea, baada ya kuvuna kura 1206.   

Mwakalebela ambaye ni Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), aliwashinda Mbunge wa Jimbo Ileje (CCM),Janet Mbena aliyepata kura(67), Yono Kevela(31), Titus Osoro(17) na Salum Chota aliyeambulia kura12.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Msola alisema ana deni kubwa la kuhakikisha klabu hiyo inapiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

“Huu ni mtahihani kwangu kufanya vizuri, kazi ya kwanza iliyoko mbele yangu ni kuvunja makundi na kuanza upya,”alisema Msola.

Kwa upande wake Mwakalebela alisema; Nimeandika historia mpya katika maisha yangu, lakini kubwa ni kufanyia kazi Yanga, nitajitahidi kadri niwezavyo kuhakikisha inafanya vizuri.

Naye Tiboroha akizungumzia kushindwa kwake alisema anaheshimu uamuzi wa wanachama wa

 Yanga na kuahidi kuendelea kushirikiana na uongozi mpya uliochaguliwa kuhakikisha klabu hiyo inapata mafanikio.

Hadi tunaenda mtamboni matokeo ya waliowania nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga yalikuwa hayajatangazwa.

Uchaguzi huo ulishuhudiwa na Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph  Singo na  Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles