30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Somalia: Polisi yazuia shambulizi la kigaidi lililopangwa kufanywa mkesha wa Ramadhani

Polisi ya Somalia imesema imetibua njama ya shambulizi la kigaidi lililokuwa limepangwa kufanywa mjini Mogadishu mkesha wa kuanza kwa mwezi wa Ramadhani hapo jana.

Naibu kamanda wa polisi Zakia Hussein Ahmed amesema afisa mmoja wa polisi ameuwawa baada ya kifaa kilichokuwa kimetegwa kwenye basi kuripuka wakati walipokuwa wakijaribu kukitegua.

Mripuko huo ambao ulitokea karibu kilomita 15 kusini mwa Mogadishu, umesikika katika mji huo mkuu.

Haijajulikana ni nani aliyehusika na kukitega kifaa hicho wala hakuna aliyetiwa nguvuni. Ulinzi umeimarishwa katika mjio huo mkuu wa Somalia huku mwezi wa Ramadhani ukiwa unaanza rasmi hii leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles