26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Pendarovski ndiye Rais mpya wa Macedonia Kaskazini

Wakili Stevo Pendarovski wa chama cha Social Democratic ndiye atakayekuwa Rais mpya wa Macedonia Kaskazini.

Wakili huyo mwenye umri wa miaka 56 amemshinda Gordana Siljanovska-Davkova ambaye ni profesa katika chuo kikuu ambaye alikuwa anawania urais kwa chama cha upinzani cha siasa za kizalendo.

Kulingana na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, Pendarovski alipata karibu asilimia 52 ya kura katika uchaguzi uliofanyika hapo jana.

Pendarovski ambaye anaelemea zaidi nchi za magharibi katika siku za hivi karibuni alikuwa mshirikishi katika harakati za nchi yake kujiunga na muungano wa kujihami wa NATO.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles