27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mpango: Waliotajwa na CAG kwenye ubadhilifu hawatosalimika

Na Clara Matimo, Mwanza

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema Serikali itawachukulia hatua viongozi wote wa umma watakaothibitika kudokoa pesa za umma kwa manufaa yao binafsi kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

Pia amewataka wafugaji nchini kubadilisha utaratibu wa kufuga waliozoea wa kienyeji na kufuga kisasa ili mifugo wanayoifuga iwe na tija kwao na taifa kwa ujumla.

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wakiwa wanamsilikiza Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango(hayupo pichani).

Dk. Mpango ameyasema hayo leo Aprili 11, 2023 kwa nyakati tofauti wakati akiwasalimia wananchi wa Kata ya Hungumalwa Wilaya ya Kwimba na Mabuki Misungwi pamoja na kutembelea mradi wa uzalishaji ngombe bora wa maziwa katika shamba la mifugo la mabuki lililopo Kijiji na Kata ya Mabuki Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo.

Amesema serikali imetoa fedha nyingi katika mikoa yote nchi nzima kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili iwanufaishe wananchi hivyo haitawafumbia macho viongozi wa umma ambao wanadokoa fedha hizo na kusababisha miradi hiyo kutekelezwa chini ya kiwango.

“Viongozi wote muwe waadilifu wa fedha za umma watakaodhibitika kudokoa fedha za miradi ya maendeleo kupitia ripoti ya CAG tutawachukulia hatua.

“Pia nawasihi sana wananchi tunzeni miundombinu ya miradi hiyo ili idumu na kutuhudumia kwa muda mrefu maana fedha zinazotumika kujenga miradi hiyo ni fedha za kodi zenu hivyo ni fedha zemu,” amesema Dk. Mpango.

Akizungumzia wafugaji kufuga kwa kisasa Dk. Mpango amesema mifugo iliyopo nchini kwa wafugaji si bora ambayo taifa linaitaka hivyp ni vyema wakatumia vituo atamizi nane vilivyopo maeneo mbalimbali nchi nzima (mashamba ya uzalishaji mifugo) ili kubadilisha ubora wa mifugo yao.

Meneja Shamba la Uzalishaji Mifugo lililopo Kata ya Mabuki Misungwi Lini Mwalla amesema shamba hilo lilianzishwa mwaka 1967 lengo likiwa ni kuzalisha ng’ombe wa maziwa, madume na mitamba bora ili kuwapatia wananchi waweze kubadilisha aina ya ufugaji.

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango (wa katikati mbele) akikagua mradi wa uzalishaji ng’ombe bora wa maziwa katika shamba la mifugo lililopo Kijiji na Kata ya Mabuki Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Amesema mradi huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uvamizi wa mifugo kutoka nje ya shamba na kuingia ndani ya shamba hivyo kupanda mifugo iliyo ndani ya shamba na kuizalisha wanyama wasio na ubora.

“Pamoja na changamoto hiyo tunaipongeza sana serikali ya awamu ya sita kwa kutuboreshea shamba hili kwani tangu lianzishwe mwaka 1967 lilikuwa halijaboreshwa lakini serikali inayoongozwa na Mheshiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetupatia ng’ombe 500.

“Kati ya ng’ombe hao wamo mitamba, ng’ombe wa maziwa na madume ambao tutawasambaza kwa wananchi ili waweze kutumia kuzalisha mitamba na madume bora hivyo kufanya ufugaji wenye tija,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles