25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

DK MAKONGORO AKUBALI YAISHE

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam


ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo na Vijana, Dk. Makongoro Mahanga, ametii amri ya Mahakama na kuanza kumlipa Mwanaharakati, Kainerugaba Msemakweli Sh milioni mbili alizoamuliwa kulipa kila mwezi.

Mahanga alifikia hatua hiyo baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa hati ya kumkamata mara kadhaa kwa kushindwa kumlipa mwanaharakati huyo kiasi hicho cha fedha, ikiwa ni sehemu ya deni la Sh milioni 11.

Mdaiwa huyo alitakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani jana lakini hakuweza kufika, badala yake mahakama ilitaarifiwa tayari alishaingiza Sh milioni mbili katika akaunti ya Msemakweli.

Msemakweli alidai mbele ya Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu, Ruth Masambu kwamba, Dk. Mahanga alishaingiza Sh milioni mbili za Februari katika akaunti yake, hivyo alitekeleza amri ya mahakama.

Alidai kwa kuwa ameanza kutekeleza amri ya mahakama, aendelee kuitekeleza bila kuwepo kwa amri ya kumkamata.

Masambu alisema wakili wa Dk. Mahanga aliieleza mahakama kwamba mdaiwa alikuwa hajaifahamisha familia yake kuhusu deni hilo, hivyo ataendelea kurejesha kama ambavyo mahakama iliamua na endapo atakiuka hatua nyingine zitachukuliwa.

Mahanga anatakiwa kumlipa mwanaharakati huyo kutokana na kesi aliyofungua ya kashfa dhidi ya mwanaharakati huyo kufutwa mahakamani.

Machi 2, mwaka huu, Mahanga alitakiwa kufika mahakamani hapo ili aweze kulipa Sh milioni mbili, zikiwa sehemu ya deni la zaidi ya Sh milioni 11 anazodaiwa na Msemakweli.

Mwaka 2009, Mahanga alifungua kesi ya madai namba 145 ya mwaka 2009 dhidi ya Msemakweli na wenzake akiwemo aliyekuwa mwandishi wa Nipashe, Muhibu Said, kwa kile alichodai kukashifiwa kutokana na mlalamikiwa huyo kuandika kitabu alichokiita Orodha ya Mafisadi wa Elimu Tanzania ambacho Dk. Mahanga alitajwa kuwa ni mmoja wa vigogo wenye shahada za udaktari wa falsafa za kughushi.

 Wadaiwa wengine walikuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe lililokuwa limechapisha habari hiyo na  Kampuni ya The Guardian Ltd

inayomiliki gazeti hilo ambapo alikuwa akiiomba mahakama kuwaamuru wadaiwa kumlipa Sh bilioni tatu kama fidia ya madhara aliyoyapata kutokana na habari hizo alizoziita za uongo. 

Hata hivyo, shauri hilo lilifutwa mahakamani hapo Julai mosi, mwaka 2014 mbele ya Jaji Salvatory Bongole, baada ya Dk. Mahanga wala  wakili wake, Kennedy Mfungamtama, kutokufika mahakamani mara kadhaa, licha ya kupatiwa hati za wito kwa tarehe zilizokuwa zikipangwa.

Kutokana na hilo, Desemba 2, mwaka 2015 mahakama ilimwandikia Mkuu wa Gereza la Ukonga barua ikiomba mchanganuo wa gharama za kumtunza gerezani mdaiwa huyo, ambapo majibu yalitoka na mahakama ilimtaka Msemakweli awasilishe mahakamani Sh 300, 000 kama kianzio kwa ajili ya

kumgharamia mdaiwa huyo kwa mahitaji ya chakula na mengine atakapokuwa amefungwa gerezani.

Msemakweli aliwasilisha fedha hizo, ambapo Mahanga alifika mahakamani hapo na kuomba alipe ambapo alikubaliwa awe anamlipa Sh milioni 2.8 kila mwezi.

Hata hivyo, Mahanga alilipa mwezi mmoja Sh milioni moja na hakuendelea kulipa tena wala kufika mahakamani. 

Januari 23, mwaka huu, mahakama hiyo ilitoa amri kwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ilala ikimwagiza kumkamata na kumfikisha mahakamani Mahanga Januari 31, ili ajieleze kwanini asifungwe jela kwa kuipuuza mahakama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles