25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

NMB MOBILE YAJA NA HUDUMA MPYA KWA WATEJA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


BENKI ya NMB imezindua huduma ya kuhamisha au kutuma fedha (NMB Mobil e Tips) kutoka katika akaunti za benki hiyo kwenda kwenye akaunti za benki nyingine.

Huduma hiyo ni ya kwanza kutolewa nchini na imetajwa kuwa ni njia rahisi, salama na ya haraka katika mchakato wa kutuma ama kuhamisha fedha kutoka NMB kwenda benki nyingine.

Akizindua huduma hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili, aliwataka Watanzania kuichangamkia huduma hiyo ili waweze kwenda na teknolojia.

Alisema huduma hiyo ni mwarobaini kwa wateja wao ambao wakati mwingine hutumia muda mrefu kwenye foleni kwa ajili ya kuhamisha ama kutembea na fedha mkononi.

“Huduma hii inakuja kumaliza tatizo la wateja wetu kutumia muda mwingi kwenye mchakato wa kuhamisha fedha. Muda ni mali na kwa kulitambua hilo, MNB tumekuja na huduma hii ambayo inafanyika popote, hata ukiwa ufukweni unapunga upepo,” alisema Adili.

Naye Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, Geofrey Mwijage, alisema benki hiyo imejizatiti kutanua huduma miongoni mwa wateja na Watanzania kwa ujumla.

Alisema NMB Mobile Tips inakwenda kuwa mshirika sahihi kwa Watanzania katika kuharakatisha maendeleo yao na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla kuelekea kwenye Tanzania ya Viwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles