30.2 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Dk. Kikwete: AGRA imeleta mageuzi makubwa sekta ya kilimo nchini

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

RAIS mstaafu wa awamu ya nne na Mjumbe wa Bodi ya Shirikisho la kuhamasisha Mageuzi ya Kijana barani Afrika(AGRA), Dk. Jakaya Kikwete amesema AGRA imeleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo nchini kwa kuwasaidia wakulima wadogo kuzalisha kwa tija kwa kuwapatia mbegu bora, teknolojia za kisasa na masoko.

Kauli hiyo ameitoa Februari 19,2022 jijini Dodoma wakazi akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ziara ya kuwatembelea wanufaika mbalimbali wa miradi  inayotetekelezwa na AGRA katika Mikoa ya Katavi, Mbeya, Songwe, Iringa.

Amesema kuwa tangu kuanza kwa Shirika hilo wamewekeza zaidi kwa wakulima wadogo na si wa kati na wakubwa na misaada ya inayotolewa ni kuwawezesha kuzalisha mazao ya chakula na biashara ya kimkakati ili nchi iwe na chakula cha kujitoshereza na wao kunufaika kiuchumi.

Dk. Kikwete amesema kuwa pia wamewekeza kutoa fedha kwa wazalishaji wa mbegu ambao watakuwa chachu ya kuhamasisha wakulima kuwa na tija ya kuzalishaji mazao kulingana na mahitaji ya Taifa na kuwepo na ziada ya chakula.

Amesema kwa Tanzania wameweza kuwafikia wakulima 6,748 ikiwa ni pamoja na kuzijengea uwezo kampuni za Wazawa 15 kwa lengo la kuhakikisha mbegu zinapatikana.

“Wanasayansi wamefanikiwa kufanya uvumbuzi wa mbegu 42 ambapo kati ya hizo 30 zimeingia katika soko. Shabaha kubwa hapa nikuwawezesha wakulima kupata mbegu na  teknolojia za kisasa.

“Kingine tumeleta karibu masoko na kwenye hili ni kusaidia baadhi ya vijiji na vyama vya ushirikika vya wakulima viwe na maghala, kuna maghala ambayo Agra imesaidia kukarabati kwa kuongezewa urefu pamoja na kuwekwa sakafu,”amesema Dk. Kikwete.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde amesema katika sehemu nyingi walizopita changamoto ilikuwa ni bei ya mbolea kuwa juu ambapo amesema wameitatua kwa kuanza ujenzi wa kiwanda katika Mkoa wa Dodoma.

Amesema kiwanda hicho kilichopewa jina la Intercom kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 600,000 kwa mwaka hivyo kumaliza tatizo la bei ya mbolea nchini.

“Ziara ya Mheshimiwa Rais nchini Burundi imetuletea tija kwani kuna wawekezaji wamekuja kuwekeza kwa kujenga kiwanda cha Mbolea hivyo tatizo la bei ya mbolea litamalizika,”amesema Mavunde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles