27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wafundishwe kujitegemea

Na Safina Sarwatt, Same

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Same Rogathe Kimario ameishauri Serikali kushirikiana na Taasisi za dini zinazotoa huduma za elimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapa elimu bora itayowaandaa kujitegemea baada ya masomo.

Askofu Kimario ameyasema hayo jana wilayani Same mkaoni Kilimanjaro katika siku ya kufungua Juma la elimu kwa shule msingi na sekondari ambazo zinamilikiwa na kanisa katoliki jimbo la Same.

Amesema kuwa serikali imezisajili shule zinazomilika na taasisi za dini kama biashara na wamiliki hao kujikuta katika wakati mgumu kuziendesha licha ya kwamba wanatoa huduma kwa watoto wa kitanzania.

“Serikali inatuunganisha kama wafanyabishara,hata zile shule zinazoaanda vijana wetu wa seminari pia serikali imeziweka kwenye kudi la shule za binafsi zinazofanyabishara, hali hii inatuweka katika wakati mgumu tunashindwa hata kuwalipa walimu.

“Sisi tunaelimisha jamii ya watanzania tunafanya huduma na kwamba utamaduni ambao hauna elimu siyo utamaduni hivyo basi tunaishauri serikali ijaribu kuzipitia shule kwani hata ada tunazotoza ni ndogo sana ukilinganisha na huduma zinatolewa,”amesema Askofu Kimario.

Amesema kuwa zipo shule za binafsi ambazo zinafanya biashara kwakutoza ada kubwa na kwamba hizo zinapaswa kuweka kwenye kudi la wafanyabiashara.

“Tumesuguana kidogo na serikali kwa muda mrefu siyo kwamba tunawekeza ili tupate fedha bali tunafanya hivyo ili jamii ya Watanzania ipate elimu bora na malezi bora tuziendesha shule hizi katika wakati mgumu,” amesema.

Meneja wa shule ya sekondari ya sayansi ya wavulana St. Joachim Padre Deogratius Mchagi amesema kuwa tupo katika kipindi ambacho dunia inahitajiwatalaamu bora walipata elimu inayoendana na mabadiliko ya teknolia ya sasa,hivyo ni jukumu la serikali kushirikiana na wadau wa elimu na kuboresha mazingira.

Amesema ni wakati wa taifa kujielekeza na kuwekeza katika utoaji wa Elimu bora na malezi mazuri kwa watoto ili kuwezesha taifa kupata wasomi wenye maadili na wazelendo kwa nchi yao.

Katibu wa elimu jimbo katoliki la Same, Laurenti Kikwesha amesema janga la uviko 19 iliyoikumba dunia imezipelekea shule hizo kupita katika hali ngumu huko baadhi ya wazazi kushindwa kulipa ada kutokana na ugumu wa maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles