24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

DK. KALEMANI: HATUTAWAFUMBIA MACHO WATAKAOKWAMISHA UJENZI BOMBA LA MAFUTA

Na SUZAN UHINGA

-TANGA

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amesema hayuko tayari kuona mchakato wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi linalotoka nchini uganda kuja Tanzania unakwama kutokana na uzembe wa mtu mmoja au taasisi itakayoshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Waziri kalemani ameyasema hayo leo wakati akifungua kikao cha siku moja cha wadau wa mradi wa bomba la mafuta ghafi linalotoka nchini Uganda hadi mkoani Tanga na kuongeza kuwa hatawafumbia macho wataofanya uzembe katika mradi huo.

Amesema lengo la kikao hicho ni kujadili mambo mbalimbali ikiwamo ushirikiswaji wa wadau katika mchakato mzima wa mradi huo mkubwa unaoghalimu Dola za Marekani bilioni 3.5 ambapo kwa nchini tanzania utapita katika mikoa nane.

“Lakini pia, mambo mengine yatakayojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na kupeana majukumu kwa taasisi zinazohusika moja kwa moja katika mradi huo na kupashana maendeleo ya mradi,” amesema.

Mchakato wa ujenzi wa mradi huo tayari umekwishaanza ambapo wataalamu mbalimbali wanaendelea na kazi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles