26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DK. KABOUROU KUZIKWA IJUMAA KIGOMA

Na Editha Karlo, Kigoma

Aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kigoma Dk. Amani Walid Kabourou aliyefariki usiku wa kuamkia leo, atazikwa Ijumaa Machi 9, mwaka huu mkoani humo.

Kwa sasa mipango ya mazishi na kusafirisha mwili huo inaendelea nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa familia, Hasna Mwilima, amesema mwili wa marehemu Dk. Kabourou utasafirishwa kesho kuelekea mkoani Kigoma ambapo atazikwa katika makaburi ya Kibampa, Shule ya Ujiji mkoani humo.

“Tumekosa usafiri wa ndege kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu hivyo inatulazimu kuzika ijumaa kwa sababu tutatumia usafiri wa barabara.

“Hii ni kwa sababu kuna msiba mwingine ambao utasafirishwa kwa ndege wenzetu hao waliwahi kufanya ‘booking’ mapema,” amesema Hasna.

Dk. Kabourou alikuwa akitibiwa katika akitokea Hospitali ya Mkoa wa Kigoma kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili mauti yalipomkuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles