29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS MAGUFULI AMLILIA DK. KABOROU

Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kigoma Dk. Amani Walid Kaburu, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Machi 7 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa, Rais Magufuli pia amesema amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Dk. Kaburu atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

“Natoa pole kwa familia yake, wana CCM wote, wananchi wa Kigoma, ndugu jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu,” amesema.

Aidha, Rais Magufuli ameiombea familia ya Marehemu na wote walioguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Dk. Kaborou alikuwa akitibiwa katika akitokea Hospitali ya Mkoa wa Kigoma kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili mauti yalipomkuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles