24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Jingu: Zingatieni uzalendo ili tuwe na takwimu sahihi

Na mwandihi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dk. John Jingu amewaasa makarani wa Sensa ya Watu na Makazi kuwa wazalendo katika zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 ili kuwa na takwimu sahihi zitakazoleta tija kwa Taifa.

Msimamizi wa Mafunzo ya Sensa Kituo cha Yombo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Wilaya ya Ubungo, Joyce Zawadi akieleza hali ya mafunzo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. John Jingu wakati alipotembelea kituoni hapo.

Ametoa kauli hiyo aliwatembelea na kuzungumza na Makarani, Wasimamizi wa Maudhui pamoja na TEHAMA katika Kituo cha Yombo kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Wilaya ya Ubungo Agosti 15, 2022.

Amesema kuwa, Serikali imewaamini kuwapa jukumu la kukusanya taarifa hizo hivyo hawana budi kuitumia fursa hiyo kwa usahihi kwa kuzingatia weledi na uzalendo wa hali ya juu.

 “Takwimu ni jambo muhimu, zoezi hili litasaidia kuwa na taarifa sahihi za takwimu zitakazosaidia shughuli za maendeleo, hata kwa wawekezaji na wafanyabiashara wetu ambao watajua namna bora ya kufanya shughuli zao zitakazochagiza katika ukuaji wa uchumi nchini,” amesema Dk. Jingu.

Aliongezea kuwa Serikali imelipa kipaumbeke suala la sensa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kulibeba jambo hilo kwa unyeti wake, maana linategemewa na taifa zima.

Washiriki wa Mafunzo ya Sensa ngazi ya Wilaya wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu (hayupo pichani) alipotembelea kituo cha Yombo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Agosti 15, 2022.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mafunzo ya Sensa katika kituo hicho, Joyce Zawadi amempongeza katibu Mkuu huyo kwa kutenga muda na kuwatembelea huku akiahidi kuendelea kusimamia mafunzo hayo kwa weledi ili kufanikisha nia ya Serikali.

“Hatutaliangusha Taifa wala Mhe. Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan tupo tayari kuleta matokeo chanya kwa maendeleo ya nchi yetu,”amesema Joyce

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles