23.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Gwajima: Rais Samia Kinara kuhakikisha wanawake hawaachwi nyuma kiuchumi

Na WAMJW – St.Petersburg-Urusi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara na kuweka ahadi katika kuhakikisha wanawake hawaachwi nyuma katika usawa wa Kijinsia na uwezeshaji kiuchumi.

Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima akiwa kati kongamano la tatu la wananwake nchini Urusi.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Oktoba 13, 2021 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima wakati akiongea na waandishi wa habari nchini hapa kwenye Kongamano la tatu la wanawake nchini Urusi.

Dk. Gwajima amesema kuwa Mhe. Rais tangu aingie madarakani ameweka ahadi ya kuhakikisha anayatazama masuala ya wanawake, haki zao na masuala ya usawa wa kiuchumi ili wasiachwe nyuma kwa sababu ya ajenda ya kijinsia ambayo huwaweka pembeni na kushindwa kuchangia maendeleo ya Taifa lao.

“Rais Samia amekuwa kinara na ameona ni vyema Tanzania tuje kusikia, kuona na kujifunza ili tusiachwe nyuma katika ajenda za kuwaendeleza wanawake na kuwa na maendeleo chanya katika nchi yao,” alisema Dk Gwajima

Aidha, Dk. Gwajima amesema kuwa, wanawake Afrika ndio wanachangia sehemu kubwa ya kufanya muonekano wa Taifa na ni walezi wa familia hivyo kongamano hilo ni muhimu katika ajenda ya kuwaendeleza wanawake hususan wanawake wa Kitanzania.

Amesema pia Kongamano la tatu la wanawake litaangalia mustakabari wa wanawake duniani katika kupewa haki na fursa sawa za kuendelea kiuchumi ili waweze kuchangia maendeleo chanya katika jamii zao.

Vile vile Dk.. Gwajima ametumia fursa hiyo kuishuruku nchi ya Urusi kwa ushirikiano na Tanzania kwa takribani miaka 60 iliyopita kwa kusaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kusomesha wataalam si chini ya 4,500 katika fani mbalimbali akiwemo yeye mwenyewe Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Tanzania inashiriki Kongamano la tatu la Wanawake Urusi ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Sulluhu Hassani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles