31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Wawili Dar, Dodoma, wajinyakulia Pikipiki za ‘NMB Bonge la Mpango’

Na mwandishi Wetu, Dar es Salaam

DROO ya kwanza ya Awamu ya Pili ya Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde inayoendeshwa na Benki ya NMB ‘NMB Bonge la Mpango – 2merudi Tena,’ umefanyika jijini Dar es Salaam leo Jumatano Oktoba 13, huku Nakaunda Baraka Mangosongo na Charles Elias Mkwizu wakiibuka washindi wa pikipiki mbili za miguu mitatu aina ya Sky Mark.

NMB Bonge la Mpango ni kampeni itakayoendeshwa kwa kipindi cha wiki 12, ikilenga kuhamasisha utamaduni chanya wa kujiwekea akiba, ambako washindi 50 watajinyakulia pikipiki za mizigo 50 zenye thamani ya Sh milioni 225, huku washindi 120 wakitarajia kujishindia fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 12.

Akizungumza kabla ya kuchezeshwa kwa droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite, alisema katika kipindi chote cha kampeni hiyo, zawadi zote zenye thamani ya jumla ya Sh. Milioni 237, zitaenda kwa washindi 170, ambao wataweka akiba katika akaunti ama kufungua akaunti mpya zenye akiba isiyopungua Sh 100,000.

“Kila wiki tutakuwa na droo za kupata washindi 12, wakiwemo 10 wa pesa taslimu Sh. 100,0000 kila mmoja, huku wengine wawili wakijishindia pikipiki za miguu mitatu (moja kwa kila mmoja), aina ya Sky Mark yenye thamani ya Sh milioni 4.5.

“Wito wetu kwa wateja wa NMB ni kuendelea kujiwekea akiba ili kujiongezea nafasi ya kushinda pesa taslimu ama pikipiki. Na kwa wale wasio na akaunti, watembelee matawi yetu yaliyotapakaa kote nchini, waweze kufungua akaunti na kuweka akiba angalau ya Sh laki moja, waingie kwenye droo hizi na kushinda,” alisema Ngingite.

Droo hiyo ilichezeshwa mbele ya Afisa toka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT), Joram Mtafya, ambaye aliwahakikishia Watanzania na Wateja wa NMB, kuwa kampeni hiyo itafanyika kwa kufuata sheria na kanuni zinazosimamia michezo hiyo na kwamba, hata akaunti za watoto walio chini ya umri wa miaka 18 (zinazoendeshwa na wazazi ama walezi), zinaweza kushinda zawadi hizo.

Ukiondoa Mangosongo na Mkwizu wa Dodoma waliojishindia pikipiki za Sky Mark, washindi wengine 10 waliojinyakulia pesa taslimu ni: Kuluthum Chande, George Fabiano, Justine Yona, Justina Mbuya na Beatrice Tarimo.

Wengine ni pamoja na: Gloriana Nicholaus, Paschal Phabian, Alphonce Donatus, Ramadhani Khalfan, Kelvin Mosha. Droo ya pili ya NMB Bonge la Mpango itafanyika wiki ijayo, kupata washindi wengine 12, wakiwemo 10 wa pesa taslimu na wawili wa pikipiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles