30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Gwajima aishukuru USAID kwa kuchangia raslimali fedha

*Chanjo ya Uviko 19 iana ya Pfizer kuwasili

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amelishukuru Shirika la Misaada la watu wa Marekani, USAID kwa kuchangia rasilimali fedha zenye lengo la kutekeleza miradi ya kuboresha huduma za Afya hapa nchini.

Aidha, ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kuiongezea Tanzania msaada wa chanjo 165,000 za aina ya Janssen ambazo ziliwasili nchini Novemba 13, mwaka huu.

Pongezi hizo amezitoa jijini Dar Salaam wakati alipokutana na Mkurugenzi mpya wa Misheni ya USAID nchini Tanzania, Kate Somvongsiri ambaye aliteuliwa kuchukua nafasi hiyo hivi karibuni. Kate amewasilisha salam za Serikali ya Marekani kwa Dk. Gwajima huku akitoa taarifa ya ujio wa chanjo zingine 500,000 aina ya Pfizer zinazotarajiwa kuwasili nchini siku chache zijazo.

Aidha, amesema kuwa serikali ya Marekani imejipanga kuisaidia Tanzania kudhibiti magonjwa yanayoambukiza ikiwemo UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na UVIKO-19 ambapo mwaka 2022 zaidi ya Sh bilioni 437 zitatolewa kutekeleza miradi ya kijamii katika kipindi cha miaka mitano kuanzia Januari, 2022 kupitia mradi unaolenga kuimarisha mifumo ya afya na uwekezaji katika jamii.

Dk. Gwajima ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kuisaidia Tanzania Chanjo milioni moja za Jansenn zilizotolewa awali pamoja na chanjo nyingine za nyongeza ambazo zitachangia kuzuia maambukizi ya UVIKO hapa nchini.

Aidha, Dk. Gwajima amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuwalinda wananchi wake kwa kudhibiti magonjwa hatarishi kama vile UVIKO hivyo ujio wa Chanjo 500,000 utasaidia kuongeza idadi ya watakaochanjwa hapa nchini

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles